Sunday, 25 August 2013

Unafahamu bidhaa inayouzwa zaidi duniani?

kama ulikuwa hujuibasi nakufahamishakuwa petrol ndiyo bidhaa inayouzwa zaidi duniani

                                                       NGOZI YA BINADAMU]

Hivi unafahamu kuwa unabadilisha leya ya ngozi yako katika mzunguko wa wiki nne?

Monday, 19 August 2013

Unamfahamu mtu anaeweza kukutanisha mabega?

 Joshua carter kutoka leesburg,Georgia anaweza kukutanisha mabega yake kama unavyomuona hapo juu na usijaribu kufanya maana ni hatari kwa maisha yako..
Joshua amezaliwa hana mifupa unayoiona hapo juu katika picha kitaalam inaitwa Collarbones

Friday, 16 August 2013

Unamfahamu kambare ana misuli mingapi?

 Kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui basi nakufahamisha..kambare ana misuli zaidi ya 100,000 ya kuonea vitu mbalimbali

                                                     UNAMFAHAMU KINYONGA?

                   Kwa taarifa yako ulimi wa kinyinga ni mrefu mara mbili ya urefu wa mwili wake

Thursday, 15 August 2013

Unamfahamu kinyozi ghali zaidi duniani?

 Salon iliyowahi kunyoa mtu nywele kwa gharama kubwazaidi duniani ni ya Stuart Philips.Gharamahiyo ni dola 16,450..piga exchange rate ya sasa 1650 unapata ni shilingi ngapi.
 Gharama hiyo ilitozwa kwenye salon hilo oktoba 29 mwaka 2007,salon hiyo ipo katika eneo la Convert Garden london nchini uingereza.

                                                     CHOCOLATE KUBWA ZAIDI

Chocolate ndefu kuwahi kutengenezwa ilipimwa na kuonekana ina uzito wa kilo 3580 sawa za daidi ya tani 3 na nusu.Chocolate hiyo ilitengenezwa Oktoba 11 mwaka 2007 na Elah Dufour wa Alessandria italia

Wednesday, 14 August 2013

Unafahamu binadamu ana misuli mingapi?

 Mwili wa binadamu una zaidi ya misuli 600 ambayo ni sawa na asilimia40 ya uzito wa mwili wake

                                                     KICHWA CHA BINADAMU

             Kichwa cha binadamu kina uwezo wa kushika misamiati ya meneno kati ya 5000 na 6000

Tuesday, 13 August 2013

unafahamu ni nchi gani watu wake wanasoma sana vitabu?

 Kama ulikuwa hujui mimi nakujuza na kukufahamisha ..kila mtu nchini Iceland anasoma vitabu vingi kuliko nchi nyingine yoyote duniani.Hebu jiulize wewe una vitabu vingapi ambavyo unavyo na kuvisoma..lakini nikikuuliza umetizama movies ngapi nadhani idadi utakuwa umeisahau kwa wingi wa movies.

                                               UTUMIAJI WA VYOO VYA UMMA

 Kwa taarifa yako asilimia 30 ya watu wanaotumia vyoo vya umma wanakataa kujisaidia huku wakiwa wamekaa kwenye vyoo vya umma.

                             UNAFAHAMU JOTO LINALOTAKIWA KATIKA MAJI YA KUOGA?

                      Joto linalotakiwa kwenye maji ili mtu aoge ni nyuzi joto 38 au fareniheiti 101

Monday, 12 August 2013

Kutokana na muonekano wake afukuzwa nchi...

 Kama ulikuwa hujui nami nakujuza na kukufahamisha..Anaitwa Omar Borkan Al Gala ambaye ni mwigizaji na pia mpiga picha huko dubai pamoja na wenzake wawili wamefukuzwa chini Saudi Arabia kutokana na kuwa na muonekano mzuri kupitiliza(handsome kupita kiasi)
Lengo la hatua hiyo imeelezwa ni kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia(kuwashobokea)dunia ina mambo jamani kama ulikuwa hufahamu sasa fahamu..sijui ukiwa na sura mbaya inakuaje saudi arabia?

Sunday, 11 August 2013

KUJITIZAMA KATIKA KIOO

kama ulikuwa hujui mimi nakufahamisha Wanawake zaidi ya asilimia 53 hawaondoki nyumbani kabla hawajajiangalia kwenye kioo na kuona urembo wao

                                                          UPINDE WA MVUA

Kama ulikuwa hujui kwa taarifa yako upinde wa mvua unaweza kuonekana asubuhi na jioni hasa jua linapokuwa lipo nyuzi 40 kutoka usawa wa nchi.

Saturday, 10 August 2013

Unamfahamu paka?.....


 Wanyama jamii ya paka hutumia asilimia 66 ya muda wao kulala na pia wana milio ya sauti zaidi ya 100

                                                       UNAMFAHAMU MBUNI?

                                  Jicho la mbuni ni kubwa kuliko ukubwa wa ubongo wake

Friday, 9 August 2013

Tafakari kauli hii...

                    NUKUU KUTOKA KWA  MZEE WETU,RAIS WA ZAMANI
                           WA AFRIKA KUSINI NELSON MANDELA
              (Msinipime kwa mafanikio bali kwa makosa niliyofanya na kujirekebisha)

                -JE UNAFAHAMU NI ASILIMIA NGAPI WATU HAWANYWI CHAI ASUBUHI?
  
Kama ulikuwa hufahamu asilimia tisa ya watu duniani hawanywi chai kwa sababu mbalimbali kila asubuhi.


                                          -KUVUNJIKA KWA MIFUPA YA BINADAMU


 kama ulikuwa hufahamu asilimia 44 ya watu duniani wamevunjika mfupa mmoja mwilini mwao.

                                                    KUTANDIKA KITANDA
kama ulikuwa hufahamu asilimia 21 ya watu duniani huamka asubuhi pasipo kutandika vitanda vyao.